Utume wa Mama Hannah (UMH) unatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha wito wa Makatekista nchini Tanzania. Tunatambua changamoto wanazokutana nazo na tunajitahidi kuwa daraja la matumaini kwao kiroho, kielimu, kijamii, na kiuchumi.
Kuratibu mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa Makatekista
Kutoa semina, mafungo, na warsha za kiroho na kitaaluma
Kutengeneza mitaala na vitabu vya mafundisho ya dini
Kutoa ufadhili wa ada kwa Makatekista wanaohitaji (moja kwa moja kwa shule/chuo)
Kutoa motisha kwa Makatekista wanaofanya vizuri katika mitihani ya kumaliza chuo
Kusaidia vyuo vya Makatekista kujiendesha kwa ubunifu na kisasa
Kushirikiana na Maparoko, Wakurugenzi wa Katekesi, na Wakuu wa Vyuo
Kutoa elimu kwa viongozi wa kiroho na walei kuhusu wajibu wao kwa Makatekista
Kujenga mahusiano mazuri kati ya Maparoko na Makatekista
Kutoa elimu ya ujasiriamali na uchumi kwa vitendo,kwa kushirikiana na Veta,Sido, taasisi ya elimu ya watu wazima na GlobalMaisha Diplomacy.
Kuhusika na maisha kamili ya Makatekista: kiroho, kimwili, kiuchumi, kijamii
Kutoa elimu na kusimamia ulinzi wa mtoto